Wabunge Bila ya kujali itikadi za vyama vyao wamelitaka Bunge
kuachana na Barua ya mahakama inayotaka kuzuia sakata la Kashfa ya fedha
katika akaunti ya Tegeta ESCROW lisijadiliwe na kutolewa maamuzi
Bungeni kwa kuwa liko Mahakamani.
Wakitoa ushauri kwa Bunge na kamati ya uongozi, Mbunge wa kigoma
kusini Mhe.Davidi Kafulila amesema mahakama imekosa uhalali mamlaka ya
kisheria na kikanuni ya kuzuia Bunge kuendelea na utaratibu wake katika
kufuatilia sakata la ESCROW.
Baadhi ya wabunge kutoka chama tawala CCM wamelitaka Bunge kuchukua
hatua kataka hilo kwa kuhakikisha taarifa ya kamati ya Bunge ya Hesabu
za serikali kuhusu wizi huo wa mabilioni ya fedha iwasilishwe bungeni.
Kwa upande wao wabunge wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA
wametaka Barua hiyo kuwekwa mezani ili kuliwezesha Bunge kumjadili
kiongozi wa mahakama kama hoja mahususi kwa mujibu wa kanuni ya 64 1e
ambaye amediriki kuingilia mamlaka ya Bunge na kulifundisha kazi zake.
Akielezea kwa ufupi hatua ya kamati ya PAC inayochunguza sakata la
ESCRO ilipofikia mwenyekiti wa kamati ya PAC amependekeza kuwepo kwa
mjadala ili kuweza kuondoa Minong’ono pamoja na kuwachukulia hatua
wahusika kwa mujibu wa sheria.
Aidha akizungumzia sakata hilo,waziri mkuu mheshimiwa mizengo pinda
amependekeza katika kutatua sakata hilo ni lazima Bunge litumie Busara
kubwa ili kuahikikisha maamuzi yatakayotolewa hayataleta hisisa za
muingiliano wa majuku na mahakama.
0 comments so far,add yours