Kamati ya kudumu ya Bunge ya hesabu za serikali imependekeza
kufukuzwa kazi kwa waziri wa nishati na madini kutokana na kulipotosha
bunge na taifa kwa ujumla kuhusiana na fedha ya akaunti ya Tegeta Escrow
pamoja na kuwa dalali mkuu aliyewakutanisha Bwana Harbinder Sigh Sing
Set na Bwaba Rugemalila katika ofisi za umma.
Akiwasilisha taarifa ya kamati kufuatia matokeo ya ukaguzi maalumu
wa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali katika akauti ya
Tegeta Escrow amesema waziri wa nishati na madini alifanya udalali huo
akijua dhahiri kuwa Bwana Sethi hana uhalali wa kisheria kufanya
biashara kwa jina la IPTL.
Kamati imependekeza waziri mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda kuwajibika
kutokana na kauli zake za kuaminisha umma kuwa fedha zile siyo za umma
kiasi kwamba vyombo vya habari ikiwemo gazeti la Daily News kuchapisha
habari yenye kichwa cha habari kilichoandika hakukuwa na tatizo katika
IPTL kauli inayoonyesha alishindwa kutekeleza wajibu wake.
Aidha mwenyekiti wa PAC Bwana Zitto Kabwe amesema kamati hiyo
inapendekeza mwanasheria mkuu wa serikali uteuzi wake utenguliwe na
afikishwe mahakamani kwa matumizi mabaya ya ofisi yaliyopelekea serikali
mabilioni ya shilingi.
Taja majina ya viongozi waliopata mgao wa fedha za Tegeta Escrow
wakiwemo viongozi wa dini na baadhi ya watumishi wa idara na taasisi za
serikali.
0 comments so far,add yours