Jeshi la polisi mkoani Mara limezima maandamano ambayo yameitishwa
na Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema wilayani Bunda mkoani
Mara,huku viongozi kadhaa wa chama hicho wakikamatwa na jeshi la
polisi kwa madai ya kukaidi amri halali ya jeshi hilo.
Askari wa jeshi la polisi wakiwemo wa kikosi cha
kutuliza ghasia wa FFU wakiwa katika magari manne tofauti walianza
kufika katika mji wa Nyasura wilayani Bunda eneo ambalo lilipangwa na
Chadema kunzia maandamano hayo, kisha kutolewa kwa amri ambayo
iliwataka wafuasi hao wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali
kutawanyika mara moja katika eneo hilo.
Hata hivyo baada ya baadhi ya wafuasi na
viongozi hao wa Chadema kukaidi amri hiyo, polisi walianza
kurusha mabomu ya machozi kisha kuwakamata watu kadhaa wakiwemo
viongozi chama hicho wilaya ya Bunda.
wakizungumzia hali hiyo baadhi ya viongozi wa
chadema wilaya ya bunda,wamelalamikiwa hatua ya jeshi la polisi
kutumia nguvu kubwa kuzima maandamano hayo ambayo wameyaita kuwa
ya amani.
Naye kamanda wa polisi mkoani Mara ACP Philip Alex
Kalangi,akizungumza kwa njia ya simu amesema jeshi la polisi
limewakamata watu kumi wakiwemo viongozi wa chama hicho wilayani
Bunda kwa kushindwa kutekeleza agizo la jeshi hilo lilowata
kusitisha maandamano hayo ya kupinga kuendelea kwa bunge la
katiba ambalo amesema linaendeshwa kwa mujibu wa sheria.
0 comments so far,add yours