Rais Jakaya Kikwete na rais Pierre Mkurunzinza wa Burundi wamezindua
mpango wa uimarishaji wa alama za mipaka ya kimataifa kati ya Tanzania
na Burundi ikiwa ni utelelezaji wa agizo la umoja wa nchi za Afrika
-AU-linalotaka nchi wanachama kuhakiki alama za mipaka kufikia mwaka
2017.
Akizungumza na mamia ya wananchi wa Tanzania na
Burundi mpakani mwa nchi hizo wilayani ngara,rais Jakaya Kikwete amesema
uimarshaji wa mipaka hauna lengo la kuwatenganisha wananchi bali kuweka
utaratibu wa huduma na usalama na kuimarisha udugu na kibiashara baina
ya nchi hizo.
Kwa upande wake rais wa Burundi Mhe Pierre
Nkurunzinza licha ya kutoa shukrani kwa Tanzania katika kuisaidia
Burundi amewatoa shaka wananchi wa Burundi walioingiliwa na mipaka na
ambapo serikali ya nchi hiyo itatafuta namna ya kuwafidia.
Awali wakizungumza katika uzinduzi huo, mawaziri wa
ardhi wa nchi hizo mbili Mhe. Prof Anna Tibaijuka na bwana Jean Cloude
Ndewayo wamesema kuwepo kwa milima na mabonde katia eneo la mipakani
kunafanya utambuzi wa mipaka kuwa migumu kwa wananchi wa kawaida kwa
kutambua tatizo hilo serikali ilianza utambuzi wa mipaka hiyo kwa
vipindi tofauti.
Uzinduzi huo uliofanyika mpakani mwa Tanzania na
Burundi uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali na nchi hizo pamoja na
wananchi wanaoishi mpakani ambapo vikundi mbalimbali vya burudani na
sanaa vilitumbwizi.
0 comments so far,add yours