Mnyumbulikaji wa Kihispania: David Silva akifunga bao la kuongoza
MABINGWA
watetezi wa ligi kuu soka nchini England, Manchester City wameanza
vyema kampeni za kutetea taji lao baada ya kuibuka na ushindi wa mabao
2-0 ugenini dhidi ya Newcastle United katika dimba la St. James Park.
Bao la
kwanza la Man City katika mechi hiyo iliyomalizika dakika chache
zilizopita limefungwa na kiungo mshambuliaji, raia wa Hispania, David
Silva katika dakika ya 39′ akimalizia vizuri pasi ya Edin Dzeko.
Mshambuliaji hatari wa Argentina, Sergio Kun Aguero aliifungia City bao la pili katika dakika za nyongeza.
Huu ni
mwanzo mzuri kwa kocha Manuel Pellegrini mwenye kibarua kizito cha
kulibakisha kombe Etihad mbele ya makocha wenzake wa kiwango cha dunia
akiwemo Louis Van Gaal (Manchester United), Jose Mourinho (Chelsea),
Brendan Rodgers (Liverpoool) na Aserne Wenger (Asernal).
Kikosi
cha Newcastle: Krul, Janmaat, Williamson, Coloccini, Dummett, Colback,
Anita (Obertan 63), Sissoko, Cabella, Gouffran (Aarons 74), Riviere
(Perez 84).
Wachezaji wa akiba: Haidara, Elliot, Steven Taylor, Abeid.
Kikosi cha Man City: Hart,
Clichy, Demichelis, Kompany, Kolarov, Fernando, Toure, Nasri (Milner
78), Jovetic (Fernandinho 73), Silva, Dzeko (Aguero 83).
Wachezaji wa akiba: Zabaleta, Caballero, Jesus Navas, Boyata.
Kadi za njano: Silva, Demichelis, Kolarov, Kompany.
Mwamuzi: Martin Atkinson (W Yorkshire)
0 comments so far,add yours