*Awasilisha mashtaka polisi
*Asema wanaomtishi watakamatwa
JESHI la Polisi limempa ulinzi wa siri Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Zitto Kabwe (CHADEMA) kama njia ya kumkinga asidhuriwe na maadui wake katika siasa.

Hatua hiyo ya polisi imechukuliwa siku chache baada ya mwanasiasa huyo kijana na mama yake mzazi, Shida Salum, kwa nyakati tofauti, kudai kuwa Zitto amekuwa akiwindwa na watu ambao wamekuwa wakitishia uhai wa wake kutokana na siasa zinazoendelea ndani ya Chadema.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi, kiliiambia RAI kuwa uamuzi huo ulifikiwa katika kikao wiki iliyopita, baada ya jeshi hilo kupata taarifa za tishio la kudhuriwa kwa kiongozi huyo kwa kile kilichoelezwa kuwa tofauti baina yake na viongozi wenzake wa Chadema.
Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours