Kufuatia tukio la watu wenye imani za kishirikina kumkata mkono mtoto
 mwenye ulemavu wa ngozi albino huko  mkoani Tabora mmoja wa waganga wa 
jadi hapa nchini Athuman Kaita ameiomba serikali kuwasaka na kuwakamata 
wahusika wote wa tukio hilo na kuwachukulia hatua kali za kisheria ili 
kukomesha unyama huo.
Akizungumza na ITV mkoani Iringa bwana Athuman Kaita maarufu kama 
dokta ngoma nzito amesema ni vema serikali ikafanya uchunguzi wa kutosha
 na kuwashughulikia wahalifu hao kama wahalifu wengine kwani unyama huo 
ni uhalifu kama ulivyo uhalifu mwingine.

0 comments so far,add yours