Sunday, July 10, 2016

LOWASSA ASHANGAZWA MIKUTANO YA KISIASA KUZUIWA

Arusha. Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ameshangazwa na polisi kuhusu uzuiwaji wa mikutano ya kisiasa akisisitiza kuwa ni kinyume cha sheria.

Kutokana na hali hiyo, ameibuka na mkakati mpya wa kuhutubia wananchi kwa kutumia mitandao ya kijamii. “Kuzuia mikutano ya kisiasa ni kwenda kinyume na sheria. Sheria imeruhusu mikutano yote ya kisiasa. Lakini hawawezi kutuzuia, sisi tutafanya mikutano na kuhutubia kwa kutumia mitandao ya kijamii na tutawapa wananchi fursa ya kuuliza maswali na tutayajibu,” amesema jana katika mkutano wa mameya na wenyeviti wa halmashauri zilizo chini ya Chadema jijini hapa. #mwananchi

Tuesday, June 28, 2016

Bet Awards

News 28 JUN: Beyoncé opened the Black Entertainment Television (BET) Awards in Los Angeles with a surprise performance of her song Freedom, with Kendrick Lamar, dancing in a pool of water. She won video of the year and the viewers' choice award for her song Formation but had already left the ceremony to catch a flight to London for a concert so her mother Tina Knowles accepted the award on her behalf.
Other winners included Taraji P Henson and Michael B Jordan, who won the acting awards. Drake won best male hip hop artist and best group with rapper/singer/producer Future, but was not at the ceremony to accept the awards. Newcomer Bryson Tiller beat Chris Brown and The Weeknd to win best male R&B/pop artist and also won best new artist. Skepta won the best international UK act. PHOTO: Danny Moloshok/ Reuters
#BBCSnapshot #photography #music #livemusic #BET @betawards

Monday, May 23, 2016

Wafugaji jamii ya Wadatoga wilayani babati wajificha vichakani kupinga kuhamishwa

vitatu wilayani Babati mkoani Manyara wakiwa na silaha za jadi mishale na mikuki wanalazimika kulala nje ya maboma yao wakipinga uamuzi wa serikali wa kutaka kubomoa maboma 11 kati ya 25 yaliyopo katika eneo la Maramboi linalopakana na mwekezaji raia wa Ufaransa kwa madai kwamba kumekuwepo na ongezeko la wafugaji ambao si wakazi wa kijiji hicho na wamekuwa wakiingiza mifugo yao katika eneo la mwekezaji huyo.
Kauli hiyo ya kupinga agizo la kutakiwa kuondoka ama kubomoa maboma yao wameitoa baada ya watendaji wa kijiji,kata na tarafa wakiwa na timu maalum iliyoandaliwa chini ya usimamizi wa polisi kufika katika eneo hilo la kijiji ili kuwashawishi kuondoka kabla ya kubomoa kwa nguvu na kwenda eneo walilopangiwa huku wakidai hawawezi kuondoka katika eneo hilo kwa kuwa agizo hilo linapingana na amri ya Mahakama ya Rufaa ya 2013 iliyowataka kuendelea kubaki hapo aidha pia wakipinga kuwepo kwa ongezeko la wageni.
Nae Katibu wa chama cha wafugaji nchini kata ya Nkaiti Bw Juma Kwanjay amesema chama hicho kinapingana na operesheni hiyo yenye muonekano wa  ushawishi ngazi ya kata kwa mujibu wa barua kwenda kwa mkuu wa wilaya hiyo badala ya kijiji,huku akidai kama lengo ni kubomoa maboma 11 na kuacha maboma 17 yaliyoamriwa na mahakama yatabaki maboma 14 kinyume na amri ya mahakama na kuchochea mgogoro huo uliokuwa umetulia.
Hata hivyo kiongozi wa oparesheni hiyo na Afisa Tarafa ya Mbugwe bw faustine Sedoyeka amesema operesheni hiyo ni utekelezaji wa agizo la mkuu wa wilaya la kuwasimamia kubomoa maboma yao na kuwapeleka eneo maalum lililotengwa lakini wamelazimika kusitisha operesheni hiyo kutokana na mazingira hayo kutokuwa rafiki kwao hasa kutokana na wafugaji hao kujificha vichakani kama mtego dhidi yao.

Friday, May 13, 2016

Makamu wa Rais amewataka viongozi wa siasa na serikali kufuata taratibu pindi wanapowawajibisha watumishi.

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu amewataka viongozi wa siasa na serikali kufuata taratibu za uwajibishwaji wa watumishi pindi inapotokea kasoro katika utendaji wao.

Akizungumza na Wauguzi na wananchi wa mkoa wa Geita katika siku ya wauguzi duniania ambapo kitaifa imefanyika katika mkoa wa Geita Mama Samia amesema serikali itaendelea kuboresha stahiki na mazingira ya kazi kila itakapoweza ili kuwafanya watumishi wa umma kufanya kazi katika mazingira bora.

 

Naye Waziri wa Tawala za mikoa na serikali za mitaa Mheshimiwa George Simbachawene amesema atasimamia na kuhakikisha haki za wauguzi zinapatikana kwa wakati ili kuboresha huduma ya afya nchini.

 

Awali akisoma risala mbele ya mgeni rasmi Rais wa chama cha wauguzi Tanzania Paul Magesa amesema mpaka sasa kuna uhaba wa wauguzi kwa asilimia hamsini na moja tu jambo hili huwafanya wauguzi kufanyakazi nyingi katika mazingira magumu hivyo kuomba ajira ziongezwe katika sekta hiyo.

Sunday, May 08, 2016

Shirikisho la wenye Viwanda waunga mkono azma ya Tanzania kuwa nchi ya viwanda

Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage  ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Wenye Viwanda Nchini–CTI,ulioambatana na kongamano kuhusu namna ya kuiharakisha  Tanzania kuwa ya Viwanda.
Katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Ukanda Maalum ya Uwekezaji –EPZA Mhandisi Joseph Simbakali,Waziri huyo amesema serikali ya awamu ya tano imejipanga vizuri kuondoa vikwazo vya uwekezaji,ikiwemo ukosefu wa maeneo ya kuweka  viwanda.
Mapema Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda Nchini–CTI Dr Samwel Nyantahe  alisema ukuaji wa  sekta ya viwanda nchini bado ni mdogo,lakini inatoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya taifa,licha ya kukabiliwa nachangamoto mbalimbali, ikiwemo gharama kubwa ya kuanzisha biashara,kodi nyingi,ukosefu wa nishati ya uhakika,wana matumaini makubwa kuwa serikali itayatatua.
Akichangia hoja Mwenyekiti wa Sekta Binafsi Tanzania-TPSF Dr Reginald Mengi amesema Tanzania itaweza kuendelea kiviwanda suala la kodi litasimamiwa vizuri, na kusisitiza kuwa ukwepaji mkubwa wa kodi na ushuru uliochochewa na uongozi mbaya ndio uliosababisha viwanda vingi vifungwe nchini katika miaka ya 80 na 90.

Akiwasilisha mada kwenye kongamano hilo Mhadhili wa Chuo kikuu Dar es salaam Prof.Lucian Msambichaka alisema maendeleo ya haraka ya viwanda nchini yatapatikana kwa kufanya kazi kwa bidii na maarifa,kuwa na sera sahihi, na utashi wa kisiasa na ushirikishwaji wa wadau wote katika 

Saturday, April 30, 2016

Wawekezaji toka nje waanza kuonyesha nia ya kutaka kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya Sukari nchini.

Wawekezaji wengi kutoka nje ya nchi wameanza kuonyesha nia ya kutaka kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya Sukari nchini baada ya rais John Pombe Magufuli kuzuia uagizaji wa sukari toka nje ili kuvilinda viwanda vya ndani.

Rais wa chama cha wanasayansi na wataalam wa Sukari na Miwa nchini (TSSCT) Mhandisi Nestory Rwechungura amesema hayo katika mkutano mkuu maalum wa wataalam hao kutoka ndani na nje ya nchi wanaokutana mjini Moshi kuweka mikakati ya nchi kujitosheleza kwa Sukari.

Mhandisi Rwechungura amesema, mikakati pia imeanza ya kuvipanua viwanda vya ndani ili kuziba pengo la uagizaji wa Sukari toka nje ambavyo vitasaidia kupanua ajira kwa vijana, kuongeza wataalam wanaomaliza vyuo vikuu na pato la taifa. 

Hata hivyo wataalam hao wamesema, wazalishaji wa Sukari nchini wakiwemo wakulima wadogo wana changamoto ya uzalishaji kutokana na kupanda kwa gharama ya teknolojia na kuifanya Tanzania kuwa na gharama kubwa ya uzalishaji katika hekta moja ikilinganishwa na nchi za Brazil, Kenya, Uganda na Malawi.

Akifungua mkutano huo mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bw Said Meck Sadiki katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na mkuu wa wilaya ya Moshi Bw Novatus Makunga amewapongeza wazalishaji wa Sukari kwa mikakati ya upanuzi wa viwanda ambao pia utawasaidia wakulima wadogo kupata soko la Miwa. 

Thursday, April 14, 2016

Waziri wa Ujenzi wa Zanzibar Balozi Karume aonya wale wenye fitina na majungu makazin

Waziri mpya wa Ujenzi, Mawasilaino na usafirishaji wa Zanzibar Balozi Ali Abeid Karume amewatahadharisha wafanyakazi wa wizara hiyo kuweka siasa pembeni na kuchapa kazi huku akiahidi hatofanya kazi kwa fitna na majungu na kuangalia itikadi za chama.
Balozi Karume ametoa tahadhari hiyo wakati wa makabidhiano ya wizara hiyo kutoka kwa waziri wa mwanzo wa awamu iliyopita  ambapo amesema huu si wakati wa kuhoji mfanyakazi anatoka chama gani ndipo apewe huduma ila ni wakati wa kuwatumikia wananchi na kuwapa huduma muhimu zote za kijamii zinazotokana na wizara hiyo ambayo inagusa hisia za watu wa rika zote.
Akizungumzia utendaji wa wizara Balozi Ali Karume amesema yeye ni mchapakazi ambaye anapenda kuwasikiliza wale anaofanyakazi nao na kuonya hatovumulia, mambo ya fitna na majungu ila anataka ushirikiano, kwa upande wake aliyekuwa naibu waziri wa wizara hiyo ya Mawasiliano Issa Haji ambaye alikabidhi kutokana na wizara hiyo kutokuwa na waziri baada ya kujiuzulu kwa Mhe Juma Duni amesema ana imani kuwa wizara hiyo mpya imepata mtaalamu na msomi na mwenye ujuzi wa kuendeleza wizara hyo.

Kikosi hicho kipya cha mawaziri wa Dr Shein mawaziri wake wamekuwa wakianza kwa kishindo na kutahadharisha kuwa huu si wakati wa siasa tena ila ni wa kuchapa kazi.

Saturday, April 09, 2016

Tshrts and Hoods available

We all Know Nobody Works Harder To stay the same. tshrts 15000 na hoods ni 30000 toa oda yako nawait oder hala at me 0718515783 au 0686720783. waoneshe kua unapenda mtu unaelekea kua kutokana na bidii zako katika kile ukifanyacho. kwa wanangu wa kweli Respost kama vip.

Tuesday, March 22, 2016

Zaidi ya kaya 1800 zakumbwa na maafa baada ya mvua kubwa kunyesha na kuezua mapaa mkoani Kilimanjaro

Zaidi ya kaya 1800 katika kata ya Machame Uroki,wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro zimekumbwa na maafa baada ya mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali kuezua mapaa ya nyumba,kungo’a miti mikubwa na migomba iliyokuwa inategemewa kwa chakula.
Wakizungumza kwa masikitiko wananchi wa kijiji cha Uswaa wamesema mvua hiyo iliyonyesha kwa muda wa nusu saa imewaacha katika hali ngumu kimaisha kutokana na mazao ya ndizi yanayotegemewa kwa chakula na biashara kuharibiwa vibaya.
Wananchi hao wamesema kuwa kutokana na hali hiyo iliyotokea katika kata hiyo, wako hatarini kukumbwa na baa la njaa huku wazee wakisema mvua kama hiyo iliyoambatana na upepo mkali iliwahi kunyesha mwaka 1986.
Diwani wa kata ya Machame Uroki Mh.Robson Kimaro amesema hali ya wananchi siyo nzuri kwa kuwa upepo huo pia umeathiri nyumba za ibada na kwamba kata hiyo inahitaji msaada wa chakula .
Kamati ya maafa ya wilaya ya Hai imelazimika kutembelea kata hiyo na kufanya tathmini ya madhara yaliyotokea ambapo mkuu wa idara ya kilimo na maafa amesema kwasasa wanatarajia kuandaa taarifa ya awali na kuiwasilisha ngazi za juu ili kuangalia uwezekano wa kusaidia wananchi hao

Sunday, March 20, 2016

Watu wasio julikana wasambaza vipeperushi vya vitisho visiwani Zanzibar.

Siku moja kabla ya kufika siku ya uchaguzi mkuu wa marudio visiwani Zanzibar hapo kesho watu wasio julikana usiku wa kuamkia leo wameziwaekea X Nyekundu nyumba kadhaa za wakazi wa Pujini katika wilaya chake chake chake na kuwaekea kipeperushi cha onyo juu ya ushiriki wao kwenye uchaguzi huo.
Moja kati ya watu walio wekewa X hizo kwenye  nyumba yake amesema wamelala walipo amka walijikuta nyumba zao zikiwa tayari zina X na kuekewa kipeperushi hicho cha onyo.

Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa Kusini Pemba ilifika kijijini Pujini Kumvini na Kijili kujionea nyumba hizo zilizo wekewa X nyekundu ampapo mwenyekiti wakamati hiyo mkuu wa mkoa Kusini Pemba Bio Mwanajuma Majidi Abdalla amewataka watu wanao taka kwenda kupiga kura waende kupiga kura na kuzipuzia X hizo huku ulinzi ukiwa umeimarishwa.

Bimwana Juma amewataka wanaume wasiwatishe wana wake kwa kutishia talaka kwa sababu ya kwenda kupiga kura badala yake wawape uhuru wanawake kuamua pindi wakitaka kwenda kwenye uchaguzi waende pasi vitisho vya vua aina yoyote.

Nae kamanda wa polisi mkoa kusini pemba kamishimna msaidi mohamed shekhan mohamed amesema jeshi lake halitishiki na vitendo vya aina hio na kwamba watawakamata wale wote waliohisika na uwekaji wa x hizo