Jeshi la polisi mkoani Simiyu linamshikilia Shabani Ernest 22 mkazi wa kijiji cha Kitongo wilayani Magu kwa tuhuma za kukutwa na noti bandia.
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi wa mkoa wa Simiyu kamishina msaidizi mwandamizi,Charles Mkumbo amesema kuwa mtuhumiwa huyo ni karani wa kampuni ya kununua pamba ya Olam ya wilayani Bunda mkoani Mara na kwamba alikamatwa juzi katika kijiji cha Mwanunui kilichoko katika kata ya Mwarushu wilayani Itirima ambapo ndipo alipokuwa akinunulia pamba.
 
kamanda mkumbo amesema kukamatwa kwa karani huyo kulitokana na kuwalipa baadhi ya wakulima pesa bandia ambao waliweza kuzingundua na kutoa taarifa kwa uongozi wa kijiji.
 
Amefafanua kuwa baada ya kukaguliwa alikutwa na noti za shilingi elfu kumi zipatazo 40 ambazo kama zingekuwa harari zingekuwa na thamani ya laki nne ambazo alikuwa akizitumia kuwalipa wakulima wa zao la pamba.
Aidha kamanda huyo ametoa wito kwa wananchi wawe macho hususani wakulima wanaouza mazao yao kipindi hiki cha msimu wa pamba kutokana na kuzagaa kwa noti hizo.
 
Pia amewaonya wafanyabiashara wanaonunua mazao ya biashara mkoani humo kuwa waaminifu na kuacha kujihusisha na biashara ya noti bandia kwa kuwalipa wakulima na kwamba jeshi hilo halitamufumbia macho mfanyabiashara wa kampuni yeyote ile atakayebainika.
 

Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours