Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Waziri Nyanga (30)  mkazi wa Tandika Dar es salaam anashikiliwa na jeshi la polisi baada ya kukutwa  na nyaraka mbalimbali za shirika la maji safi na maji taka Dawasco huku akifanya kazi za kukatia wananchi maji na kukusanya mapato.
Mtu huyo alikutwa na nyaraka hizo zikiwamo Tisheti, Kofia, Karatasi mbalimbali pamoja na stakabadhi na vifaa vya kukatia maji endapo mtumiaji wa maji hakulipa bili huku akikosa uhalali wa kufanya hivyo kwakuwa hatambuliki na uongozi wa Dawasco na pia hakuwa na kitambulisho kinamchomtambulisha kuwa ni mfanyakazi wa shirika hilo.
 
Uchunguzi uliyofanywa ulibaini mtuhumiwa alikuwa akifanya shughuli hizo kwa miaka mitatu na alikuwa akitoa stakabadhi kwa waliyolipa na kukata maji kwa waliyokosa fedha na alipopekuliwa nyumbani kwake alikutwa na nyaraka hizo na kufikishwa kituo cha polisi Chang'ombe.

Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours