Mkuu wa wilaya ya Karatu mkoani Arusha Bw Felexs Ntebenda  amewatakata wananchi wa wilaya hiyo kutoa ushirikiano wa  kuwezesha kukamatwa  kwa  kikunadi  cha watu  kinachoendesha  vitendo vya hujuma kwenye miradi ya maji na umeme inayotekelezwa katika maeneo mbali mbali ya wilaya  hiyo.
Bw  Ntebenda  ameyasema  hayo  alipokuwa  akizungumza  na  wananchi  wa  kata ya  Endamarieki juu ya kuwepo  kwa  watu  wanao  haribu miundombinu ya maji  na kuhamasisha  wananchi  kudai  fidia   zisizo za lazima kwenye  miradi  inayotekelezwa kwenye maeneo yao.
 
wakizungumzia  changamoto hiyo baadhi ya  viongozi akiwemo  mbunge  wa karatu Mh Israel Natse wamewataka wananchi kutambua  kuwa  miradi  yote inatekelezwa kwa kodi zao hivyo wanapoona mtu  anaharibu anachezea fedha na nguvu  zao. 
 
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wamesema miradi mbalimbali  ikiwemo ya ,maji na umeme inayotekelezwa kwenye maeneo yao  imeanza kuwapunguzia makali ya maisha.

Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours