Mtu mmoja ambaye hajatambulika amekutwa ameuwawa kwa kuchomwa chomwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kitu chenye incha kali  katika makaburi ya misuna Singida mjini.
Wakielezea tukio hilo balozi wa mtaa wa mwenge Bi. Mary Mwambusu   na mwenyekiti wa mtaa wa misuna Bwana Sarota Masawe wamesema  tukio hilo linaonekana kutokea  majira ya alfajiri  ya siku ya tarahe tano mwezi wa nane katika makaburi ya misuna.

Viongozi hao wa mtaa Mwenge na Misuna wamesema tukio hilo ni la kwanza kutokea  lakini wameliomba jeshi la polisi kuimarisha ulinzi hasa maeneo kama hayo ilikudhibiti mauaji kama hayo yasi tokee tena.

Akiongea kwa njia ya simu kamanda wa jeshi lapolisi mkoani Singida  Bwana Geofrey Kamwela amekiri kutoke kwa tukio hilo katika eneo la makaburi yaliyopo  misuna Singida mjini na amesema jeshi lake bado linaendelea na uchunguzi kuweza kubaini chanzo cha mauaji hayo ambayo ni ya kinyama.



Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours