Dodoma  
Kambi ya Upinzani Bungeni imeishauri serikali kutojiingiza katika usimamizi na uendeshaji wa shughuli za ushirika nchini, kwa kuwa hatua hiyo inaenda kinyume na misingi ya ushirika na inaondoa mamlaka ya wanaushirika.
 Akiwasilisha maoni ya kambi hiyo bungeni mjini Dodoma, kufuatia kuwasilishwa kwa muswada wa sheria ya vyama vya ushirika, mbunge wa viti maalum (CHADEMA) Bi. Rose Kamili Sukum, amesisitiza kuwa serikali haiwezi kuwa mtendaji mkuu kwenye ushirika, kwa kuwa utendaji wa ushirika hauna tofauti na sekta binafsi.
Nayo, Kamati ya bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, kupitia kwa Makamu Mwenyekiti wake, Mbunge wa Sikonge, Bw. Said Nkumba, imetaka kufutwa kwa chama kilele cha ushirika, kwa kuwa kinaongeza mzigo kwa wanaushirika.
Aawali akiwasilisha muswaada huo wa sheria ya vyama vya ushirika nchini, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Eng. Christopher Chiza, amesema kutungwa kwa sheria hiyo, kumetokana na azma ya serikali kufufua na kuimarisha sekta ya ushirika nchini.
Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours