*Rais Kagame aing’ang’ania Tanzania
*Apandisha ushuru kwa asilimia 200

NI dhahiri sasa biashara ya kupitisha mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam, imekuwa moto, baada ya Serikali ya Rwanda kupandisha tozo ya ushuru kutoka dola za Marekani 152 hadi 500 ambazo ni sawa na Sh 800,000 za Tanzania.

Hali hii inawezekana kwa namna moja au nyingine, imetokana na mzozo kati ya Rais Jakaya Kikwete na Rais Paul Kagame wa Rwanda, ambao umepelekea wafanyabiashara wa Rwanda na Uganda kutishia kuacha kupitisha mizigo yao katika Bandari ya Dar es Salaam.

Itakumbukwa mzozo huo, umekuja baada ya Rais Kikwete kumshauri Rais Kagame akubali kukutana na waasi wanaoendelea na vita mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), lakini ushauri huo unaonekana kupokelewa tofauti na Rais Kagame.

Siri ya kupandishwa kwa gharama hizo, imefichuka jana baada ya malori mengi ya wafanyabiashara wa Tanzania kukwama katika mpaka wa Rusumo mkoani Kagera.

Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours