wadau wa matumizi bora ya ardhi wamesema tatizo la ongezeko la migogoro ya ardhi kati ya wakulima wafugaji na maeneo yaliyo hifadhiwa halitaweza kumalizika kama serikali hawatatilia mkazi upimaji ya mipaka na mpango wa matumizi bora ya ardhi.
Kauli hizo zimesemwa na watalam wa ardhi na wadau wengine wa matumizi bara ya ardhi katika kikao kilicho wakutanisha watalam wadau na kamishina wa ardhi kanda ya kaskazini kujadili changamoto ya ongezeko la migogoro ya ardhi kati ya jamii za wakulima wafugaji na maeneo yaliyo tengwa kwa ajili ya matumizi maalum.
Kamishina msaidizi wa ardhi kanda ya kaskazini Suma Tumpale amesema tofauti na maeneo mengine kanda ya kaskazini imekuwa na migogoro mingi ya ardhi inayo tokana na kutokuwepo kwa mipango ya matumizi bora ya ardhi huku afisa wa ardhi kutoka halmshauri ya Simanjiro Baltazal Sule akidai wilaya simanjiro imeanza kupunguza tatizo ilo kwa kupanga matumizi bora ya ardhi.

Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours