Serikali imekipongeza kiwanda cha  vinywaji baridi ya bonite ya moshi kwa kutekeleza kwa vitendo usimamizi wa sheria katika uzalishaji wa bidhaa zenye kukidhi viwango vinavyokubalika na hifadhi ya mazingira bila kuathiri jamii inayoizunguka kiwanda hicho.

Naibu waziri wa nchi,muungano na mazingira Bw.Luhanga Mpina ametoa pongezi hizo wakati alipotembelea kiwanda hicho na kujionea hali ya uzalishaji wa bidhaa zake zikiwemo soda za aina mbali mbali na maji.
Bw mpina amesema, pamoja na suala la kukidhi viwango vya uzalishaji wa bidhaa hizo kiwanda hicho pia kinazingatia suala la hifadhi ya mazingira na kuwa mfano wa viwanda na makampuni  ambayo ameyataka kweda kujifunza bonite.
Mratibu wa baraza la taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira (NEMC) kanda ya kaskazini Dr.Menar Jangu amesema,kiwanda hicho kila walipokitembelea hata kwa kushtukiza walikuta kila idara ipo katika mazingira mazuri ya uzalishaji wa bidhaa zake.
Meneja wa masoko na mauzo wa kiwanda hicho kanda ya kaskazini Bw.Christopher Loiruk amesema,Bonite tangu ianze uzalishaji wa bidhaa zake imekuwa ikizalisha bidhaa zinazokidhi viwango vya kimataifa mwaka hadi mwaka.

Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours