
Mashirika mbalimbali na watanzania 
kwa pamoja wameombwa kuwa na utamaduni wa kuchangia  na kuboresha shule 
maalumu ambazo zina walemavu wa ngozi ,badala ya kusubiri matukio ya 
uvamizi kutokea na kuanza kuchukuwa hatu ,kwa kufanya hivyo kuta saidia 
walemavu  wa ngozi kupata elimu bila ya kuwa na wasiwasi ya kuvamiwa na 
baadhi ya watu wenye nia mbaya.
 
 
Mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Parseko Vicent Kone amesema hayo katika
 hotuba yake iliyo somwa na mkuu wa wilaya ya Singida, Bwana  Said 
Amanzi katika  hafla ya kukabidhi mradi wa uboreshaji wa miundombinu 
rafiki kutoka shirika la Koica la nchini korea,na kusema kuwa mashirika 
kutoka  mataifa  mengine wame weza kuchangia na sisi watanzania   
inatubidi kuchangia kwani jukumu la kuwalinda walemavu wangozi ni ni la 
watanzai wenyewe na kuhakikisha wana pata  ulinzi na elimu kama watu 
wengine.
Kwa upande wake  meneja mradi wa kujitolea kutoka shirika la Koica 
nchini korea  Bi. Park Jieun amesema mradi wa uboreshaji  wa miundombinu
 katika chuo cha ufundi na marekebisho kwa watu wenye ulemavu sabasaba 
umegarimu zaidi ya shilingi milioni arobaini na mbili kwa ajili ya 
kuboresha mazingira ya chuo kwa kujenga mabweni,matanki ya maji na 
kuwasaidi walemavu  ili waweze kuishi kama watu wengi ambao siyo 
walemavu.
Awali mkuu wa  chuo cha ufundi na marekebisho kwa watu wenye 
ulemavu cha sabasaba Bi. Fatuma Malenga ameiomba serekali kuangali 
uwezekano wa kukijengea uzio chuo na kuweka  vivuko maalumu pamoja na 
alama katika barabara ambayo ipo karibu na chuo ili kuwawezesha wenye 
ulemavu wa ngozi na walemavu wengine kuishi katika mazigira salama. 

0 comments so far,add yours