Chama cha demokrasia na maendeleo -Chadema kimewataka watanzania kutambua, dawa ya migomo na migogoro kwenye sekta mbalimbali inayoendelea nchini ni kuiondoa CCM madarakani kupitia umoja wa katiba wa wananchi–UKAWA kwenye uchanguzi mkuu ujao, kwa kuwa imeshindwa kuyatafutia ufumbuzi matatizo ya wananchi.
Hayo yamesemwa na naibu katibu mkuu wa chama hicho John Mnyika kwenye mkutano wa uchanguzi wa viongozi wa kanda ya kusini wa chama hicho uliofanyika mkoani Mtwara, na kuhudhuriwa na viongozi wa ngazi mbalimbali wa Chadema toka mikoa ya Mtwara na Lindi, katika kutekeleza sera ya majimbo kwa mujibu wa katiba mpya ya chama hicho ambapo ulichagua mwenyekiti wa kanda, makamu mwenyekiti, mratibu wa kanda, afisa wa kanda na kamati 6 za utendaji za kanda hiyo ya kusini katika kuimarisha chama na kujiandaa na uchaguzi mkuu ujao.
 
Naibu katibu mkuu huyo wa Chadema John Mnyika amesema, taifa linapita kwenye migogoro na migomo inayoathiri uchumi na ustawi wa wananchi, na hivyo dawa ya kumaliza migomo na migogoro hiyo ni kuiondoa CCM madarakani kwenye uchaguzi mkuu ujao huko akidai umoja wa katiba ya wananchi - UKAWA ipo imara kutekeleza matarajia ya wananchi katika kushinda uchaguzi mkuu ujao.
 
Aidha baadhi ya washiriki wa mkutano huo wa uchaguzi wamewataka wanachama wa chama hicho kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la kupigia kura wakati utakapowadia, ili kufanikisha malengo ya chadema na umoja wa katiba ya wananchi ukawa wa kushinda kwenye uchaguzi mkuu ujao yaweze kufanikiwa.
Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours