Wakazi wa jiji la Dar es salaam wametakiwa kuwa makini kutokana na 
kuwepo kwa vishoka wa wizi wa maji wanaojifanya kuwa ni wafanyakazi wa 
wizara ya maji chini ya shirika la maji safi na maji taka DAWASCO ambao 
wamekuwa wakiingia mikataba ya kitapeli na baadhi ya wananchi kwa 
kuwaunaganishia maji ya wizi na kuwasababishia matatizo.
Kadhia hiyo imemkumba mkazi wa mabibo EXTERNAL Bwana.Saidi Juma 
ambaye amefungiwa maji kitapeli kutoka mabibo na kijana alifahamika kwa 
jina la Rajab Mrisho ambaye alimdanganya mzee huyo kuwa ni mfanyakazi wa
 DAWSCO na kumuunganishia maji hayo kutoka kwenye bomba lingine la 
mabibo kwa mkataba wa kulipa elfu hamsini kila mwezi.
Waunganishaji wa maji kwa kutumia ujanja ujanja wamekuwa 
wakirudisha maendeleo nyuma na kuwatia hasara watu wanao waunganishia 
huduma hiyo bila kibali maalumu ambapo inakuwa ni hatari na hivyo 
kuchafua jina shirika la maji safi na maji taka DAWASCO nakuonekana kuwa
 niwalaghai katika utoaji huduma kumbe sio sahihi.

0 comments so far,add yours