ABIRIA 13 wakiwemo watatu wa familia moja wamefariki dunia mkoani Singida leo, baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina
ya Noah T.730 BUK, kugongwa na Lori aina ya Scania.
Ajali hiyo ya kusikitisha imetokea leo saa1.32 asubuhi katika barabara kuu ya Singida-Dodoma eneo la kijiji cha Isuna tarafa ya Ikungi wilaya ya Ikungi mkoani Singida. Kamanda wa polisi mkoa wa Singida,SACP ,Geofrey Kamwela, amesema gari hilo aina ya Noah lilikuwa likitokea Itigi wilaya ya Manyoni na lilikuwa na safari ya kuja Singida mjini.Amesema hadi sasa miili ya abiria 10 wamekwisha tambuliwa na ndugu zao na miili ya abiria watatu,bado haijatambuliwa na miili yote bado imehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali
ya mkoa mjini Singida

Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours