Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete 
amefanya mabadiliko ya wakuu wa wilaya ambapo amewateua wakuu wa wilaya 
27 wapya na 64 kuhamishwa kwenye vituo vyao vya awali huku akitengua 
uteuzi wa wakuu 12 na wengine 7 kupangiwa majukumu mengine na waliobaki 
42 wakisalia kwenye vituo vyao vya sasa.
 
 
Akitoa taarifa ya mabadiliko hayo kwa niaba ya rais waziri mkuu wa 
jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe Mizengo Pinda amesema katika nafasi
 27 ambazo wameteuliwa wakuu wa wilaya wapya zimetokana na sababu 
mbalimbali ikiwemo kufariki dunia kwa wakuu wa wilaya watatu, 
kupandishwa kwa wakuu watano kuwa wakuu wa mikoa, saba kupewa majukumu 
mengine ambapo hapa anataja baadhi ya majina ya wakuu walioteuliwa huku 
kukiwa na sura nyingi mpya za vijana.
Waziri mkuu pia akataja majina ya wakuu wa wilaya 12 ambao uteuzi 
wao umetenguliwa na rais kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo umri na 
matatizo ya kiafya ambapo miongoni mwa majina mashuhuri ni pamoja 
aliyekuwa mkuu wa wilaya ya kiteto martha umbula, james ole Millya 
Longido na Elibariki Emmanuel Kingu aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Igunga.
Mhe waziri mkuu amebainisha kuwa mabadiliko hayo yanaanza kazi mara
 moja huku wakuu wapya 27 wakipatiwa semina maalum ya uongozi na namna 
ya kutekeleza majukumu yao itakayotolewa na ofisi ya waziri mkuu tawala 
za mikoa na serikali za mitaa.


0 comments so far,add yours