Mkuu wa mkoa wa tabora BW. RUDOVICK mwananzira, amesema vifo vya
akinamama na watoto vinaweza kuzuilika, kama kila mmoja atatimiza wajibu
wake, ambapo amemuagiza mganga mkuu wa mkoa huo kuvitolea maelezo vifo
hivyo kutokana na kupanda na kushuka kila mwaka na atabainika
aliyehusika hatua zichukuliwe dhidi yake.
Bw. Rudovick Mwananzira anetoa kauri hiyo wakati akizungumza na
wadau wa afya mkoani Tabora, katika akizindua mpango mkakati wa
kupunguza vifo vya akinamama na watoto, pamoja na kutathimini maendeleo
ya kupunguza vifo hivyo ambapo amebainisha kushindwa kufikia lengo la
chini ya vifo theruthi mbili mwaka 2015,
Aidha amesema kuwa, lengo lililowekwa la kupunguza vifo kutoka
112/100,000, kufikia 90/100,000, mwaka 2013, halikufikiwa na matokeo ya
vikaongezeka mpaka 117,/100,000, 2014, na hivyo unahitajika uwajibikaji
ili kufikia lengo lililokusudiwa, na hatua za makusudi zichukuliwe
ikiwemo kuwajibishana.

0 comments so far,add yours