Mbunge wa Mbinga Magharibi Mh.
Kapteni John Komba amefariki Dunia leo
saa 10 jioni katika Hosptali ya TMJ
Mikocheni.
Kwa Mujibu wa mtoto wa Marehemu Bw.
Jerry Komba amesema kifo cha marehemu
baba yake kimetokana na ugonjwa wa
kisukari ambapo amedai kuwa sukari
ilishuka ghafla akiwa nyumbani kwake
Mbezi Beach Dar es salaam.
Katibu wa mbunge huyo Bwana Gasper
Tumaini amesema kuwa mbunge huyo
alikimbizwa katika hospitali ya TMJ
ambapo ndipo mauti yamemkuta.
Aidha Bwana Gaspaer Tumaini ameongeza
kuwa mwili wa marehemu umehamishiwa
katika hosptali ya Lugalo jijini
Dar es salaam ambapo ratiba ya Mazishi
bado haijafahamika.
Eatv imewatafuta Afisa habari wa Ofisi ya
Bunge ndugu Owen Mwandumbya,
Mkurugenzi wa Mambo ya nje na Elimu
kwa umma bwana Jesse Mwakasyuka na
katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashilila
bila mafanikio kwa kuwa hawakupokea
simu
Source:eatv.tv

Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours