Jumuiya ya wanataaluma wa chuo kikuu 
cha Dar es salaam kwa kushirikiana na  ITV/REDIO ONE wamekubalianan 
kuandaa  midahalo ya wagombea urais kuelekea katika uchaguzi mkuu wa 
mwaka huu ambapo itv/redio one watakuwa wanarusha midahalo hiyo mja kwa 
moja.
Makubalinia hayo yamefanyika jijini dar es salaam baina ya 
 mkurugenzi mtendaji  wa ITV/Redio One Joyce Mhavile na mwenyekiti wa 
udasa Profesa Kitilya Mkumbo ambapo mwenyekiti  huyo amesema uwepo wa 
midahalo hiyo ni  nafasi nzuri kwa wagombea kunadi sera  zao.
Kwa upande wake mkurugenzi wa ITV /Redio One amesema wao kama kityo
 cha  habari wanaamini midahalo hiyo ni  nguzo imara kwa wasomi kuweza 
kuchambua  hoja za wagombea kabla ya kufanya maamuzi ya kuwachagua ama 
la,Kama  ilivyo ada katika mikutano baadhi ya waandishi w habari 
walipata nafasi ya kuuliza  maswali mbalimbali na kupatiwa  majibu  na 
meza kuu.

0 comments so far,add yours