Serikali imesema matukio ya ugaidi na uharamia yanayoendelea katika 
ukanda wa Afrika ni changamoto kubwa katika nchi kwa sasa hivyo 
kunahitajika jitihada za maksudi katika kukabilina na matukio hayo.Waziri wa nchi ofisi ya rais serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Mh.Haji Omar Kheir ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya awali ya askari polisi na uhamiaji katika chuo cha taaluma ya polisi Moshi.
Amesema katika kukabiliana na matukio hayo askari polisi hapa 
nchini hawana budi kuimarisha mahusiano mazuri na wananch sanjari na 
kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia misingi ya haki za binadamu ili 
iwe rahisi kupata taarifa za wahalifu wa matukio hayo ambayo 
yanahatarisha amani.
Kwa upande wake mkuu wa jeshi la polisi nchini Igp Ernest Mangu 
amesema pamoja na takwimu za mwaka 2014  za kupima viwango vya uhalifu 
na usalama duniani kuonyesha Tanzania ni nchi ya kwanza katika ukanda wa
 afrika mashariki na kusini mwa afrika kuwa salama, bado kuna matishio 
kadhaa ambayo yameanza kujitokeza na  kuhatarisha amani na usalama 
katika nchini. 
Naye mkuu wa chuo cha taaluma ya polisi moshi (MPA) afande Matanga 
Mbushi amesema jumla ya askari polisi na uhamiaji 3210 wamehitimu 
mafunzo hayo na wengine 299 waliachishwa mafunzo hayo kutokana na utovu 
wa nidhamu ikiwemo kugushi vyeti kwa ajili ya kujiunga na jeshi hilo.
Katika hafla hiyo pia askari hao wameonyesha umahiri na ukakamavu 
wa hali ya juu katika kukabilina na wahalifu kwa kuonyesha mazoezi ya 
vikwazo. 

0 comments so far,add yours