Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na baba yake mdogo kupitia East Africa Radio leo asubuhi, mazishi ya rapper Albert Mangwea aliyefariki jana katika hospitali ya St. Helen jijini Johannesburg, Afrika Kusini yanaweza kufanyika mjini Morogoro.

“Tumekubaliana kwamba tumelazimika kuzika Morogoro kwasababu huyu kaka yetu ambaye ni baba wa marehemu tumemzika pale Morogoro na familia yote ya marehemu ipo pale Morogoro. Lakini hapa Dar es Salaam tutafanya mapokezi na msiba utakuwa hapo kwa kaka yangu ni sehemu za Mbezi hapo, kwahiyo tutakuwa kwa kaka yangu anaitwa David Mangwea,”amesema.

Ameongeza kuwa taarifa hizo za msiba nao walizipata jana jioni lakini bado hawajawa na uhakika ni vipi mwili wa marehemu utaletwa nchini kutokea Afrika Kusini.

“Kitu tunachokifanya na tumewaagiza tu hao vijana wetu waliopo hapo Dar es Salaam wajaribu kuwasiliana na ubalozi wa Afrika Kusini kuona namna gani ambavyo tunaweza kupata more information na kiasi kwamba tukaweza kujua namna gani msiba utakuja hapa.” 
Mpaka sasa bado haijajulikana mwili wa marehemu Mangwea utakuja lin.
Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours