Tunaomba radhi kwa watu wote ambao mlikuwa mmeshanunua tickets za miaka 13 ya Lady JayDee ambapo onyesho ilikuwa lifanyike Ijumaa ya tar 31 May 2013.
Tunapenda kuwataarifu kuwa onyesho hilo limesitishwa kutokana na msiba mzito wa msanii mwenzetu Ngwair mpaka hapo tutakapo wataarifu tena.

Tunasubiri taratibu za kuupokea mwili na tarehe ya maziko, baada ya hapo tutaendelea na ratiba za show na tutawatangazia tarehe inayofuata ambayo si mbali baada ya maziko.

Wale mliokwisha nunua tickets naomba mzitunze tickets zenu, kwani ndio hizo hizo mtakazozitumia siku ya show hata kama tarehe imebadilishwa.

Natanguliza shukrani na naomba radhi kwa usumbufu wowote nitakaokuwa nimewasababishia.
Kila kitu kitaendelea kama kilivyokuwa kimepangwa, hapo baadae
Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours