UMOJA wa Walemavu Waendesha Bajaji jijini la Dar es Salaam, wamemwomba Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita,  kuhakikisha wanapatiwa vituo vya kufanyia biashara zao ili kuondokana na adha wanazopata za kulipishwa faini.
Akizungumza jana katika mkutano ulifanyika katika ukumbi wa Karimjee, Mwenyekiti wa umoja huo,  Nyaikoba Msabi alisema kwa kipindi kirefu polisi wamekuwa wakiwanyanyasa bila kujali hali waliyokuwa nayo.
“Tunanyanyasika, polisi wanatutoza  faini bila kujali hali tuliyonayo, hatukuomba kuwa hivi, tumeamua kuondokana na suala zima la ombaomba kwa kuamua kufanya biashara ya bajaji, lakini bado polisi wamekuwa wakitunyanyasa, tunaokumba utusaudie kwa hili,” alisema Msabi.
Aliongeza kuwa mbali na changamoto hiyo , lakini pia kilio kingine ni kukosa ruhusa ya kuingia kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa jambo ambalo linawafanya kurudi nyuma kimaendeleo katika kujitafutia riziki.
Kwa upande wake Meya wa Jiji hilo Isaya Mwita, alisema amesikia changamoto hizo na kwamba atafanya kila njia kuhakikisha kwamba wanapatiwa vituo kwa haraka.
“Wananchi wanatakiwa kuwathamini watu wenye ulemavu kwa kuwa wanahitaji kuthaminiwa kama ilivyo kuwa kwa wananchi wengine.

Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours