ALAAM
BARAZA la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), limethibitisha kuwa Kenya itakua mwenyeji ya michuano ya Kombe la Chalenji na michuano ya klabu bingwa (Kagame).
Michuano ya Chalenji imepangwa kufanyika Novemba mwaka huu, huku ile ya klabu imepangwa kufanyika Desemba ambayo ndiyo itaathiri Ligi Kuu Tanzania Bara.
Ligi Kuu Tanzania Bara Desemba inakua katika mzunguko wa pili, tofauti na Kenya wanakuwa katika mapumziko baada ya ligi kumalizika, hivyo kuondoka kwa Yanga kutaathiri ratiba.
Katibu wa Cecafa, Nicholaus Musonye, alinukuliwa na Mtandao wa Futaa akisema Kenya ambao ni wenyeji watawakilishwa na timu mbili za Gor Mahia na Ulinzi Stars.
“Tunafikiria kuwa na timu tatu, lakini nyingine itaingia baada ya kuona zile timu zilizoalikwa kama zitathibitisha ushiriki wao.
“Tunafikiria Kenya wataandaa mashindano mazuri kuliko yale yaliyowahi kufanyika,” alisema.
MTANZANIA lilimtafuta Katibu wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Celestine Mwesigwa, kujua kama wana taarifa hizo, ambapo alijibu hawakua na taarifa za mashindano hayo yote kufanyika Kenya.
“Niliongea na Musonye siku za karibuni, alichonieleza ni kuwa Chalenji itafanyika Sudan, hii ni taarifa mpya bado sijaipata,” alisema.
Kagame awali ilipangwa kufanyika Juni na Julai mwaka huu Zanzibar, baadaye mashindano hayo yalihamishwa ili yafanyike Tanzania Bara kutokana na Zanzibar ilikuwa imetoka katika uchaguzi, hivyo isingeweza kuwa mwenyeji lakini Bara napo yalishindikana baada ya TFF kusema hawakua wamejiandaa kuwa mwenyeji.
Hata hivyo, mashindano hayo yalishindikana kufanyika kwa muda uliopangwa baada ya kukosa nchi mwenyeji.
Mara ya mwisho Kenya kuwa mwenyeji wa Kagame ni mwaka 2001, ambapo Tusker ilikua mabingwa, pia nchi hiyo mara ya mwisho kuwa mwenyeji wa michuano ya Chalenji ni mwaka 2013 ambapo wenyeji hao walichukua kombe.
Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours