Ni August 12, 2016 ambapo kupitia kampuni ya Anuflo Industries imezindua Believe disposable seat cover na Blotting paper ambazo zitatumika kwenye matumizi ya binadamu.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Mkurugenzi wa bidhaa hizo Flora Christandus alisema>>>‘Believe disposable seat cover itasaidia
hasa pale mtu anapohitaji kwenye toilet kisha ataiweka pembezoni kabla
ya kukalia choo hicho ili kuzuia magonjwa mbalimbali baada ya kumaliza
matumizi ya hiyo Disposable seat cover utairuhusu iende na maji‘-
‘Ya pili ni Blotting paper
ambayo itatumika hasa mtumiaji anapotaka kuondoka make up usoni au
jasho lake kwahiyo badala ya kutumia kitambaa unaweza ukatumia Blotting paper hizi bidhaa zitaanza kupatikana madukani‘- Flora Christandus
Hizi ni baadhi ya picha kutoka kwenye uzinduzi huo uliofanyika Terrance Lounge My Fair Plaza.
0 comments so far,add yours