Mtoto wa John Kennedy, JFK Jr., akirusha angani ndege yake, alitoweka bila kujulikana alikokuwa na hatimaye kukutwa amekufa pamoja na abiria wake wawili waliokuwa katika ndege hiyo. Mmoja wao alikuwa mchumba wake. JFK Jr., alifariki Julai 16, 1999 (tazama hizo tarehe). Baada ya kupatikana maiti yake ilichukuliwa na kuzikwa upya.
John Kennedy na Abraham Lincoln, wote, kwa nyakati tofauti, walisoma sheria na wote waliwahi kufanya kazi jeshini.
Kennedy alichaguliwa kuwa Rais Novemba 8. Lincoln alichaguliwa kuwa Rais Novemba 8. Kennedy alikuwa mtoto wa pili katika familia yake. Lincoln naye alikuwa mtoto wa pili katika familia yake.
Wote wawili walitumia majina ya babu zao. Kennedy alikuwa na watoto walioitwa Robert na Edward, kadhalika Lincoln alikuwa na watoto walioitwa Robert na Edward. Kennedy alizaa watoto wanne, na Lincoln alizaa watoto wanne.
Lincoln alikuwa na daktari wake aliyeitwa Charles Taft. Kennedy naye alikuwa na daktari wake aliyeitwa Charles Taft. Lincoln alikuwa na rafiki na mshauri aliyeitwa William Graham. John Kennedy alikuwa na rafiki na mshauri aliyeitwa Billy Graham. Inasemekana kuwa Billy na William ni majina mawili yanayotofautiana katika kuandikwa lakini si katika maana.
Chanzo kimoja cha habari kinasema kuwa mwaka mmoja kabla Lincoln hajauawa alipokea barua 80 zilizotishia maisha yake. Kadhalika, chanzo hicho hicho kinasema, mwaka mmoja kabla ya kuuawa Kennedy alipokea barua 800 za kutishia uhai wake. Barua za kennedy ni mara kumi ya zile za Lincoln, lakini namba yake ni nane.
Lincoln aliuawa mbele ya mkewe na Kennedy aliuawa mbele ya mkewe. Wake zao hawakudhurika wakati wa mauaji ya waume zao. Orodha hiyo inaweza kuendelea hadi ukachoka ila Leo niishie hapa.... sijui kwanini ilitokea hii.
Credt:vyanzo mbalimbali mtandaoni.#wikipidia
Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours