Taarifa ninayokusogezea ni ya David Kafulila aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kusini, tunafahamu ana kesi Mahakamani ya kupinga matokeo ya ubunge 2015jimbo la Kigoma Kusini kesi ipo Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, taarifa ikufikie kuwa Kafulila baada ya kufika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma akasomewa kesi mpya ambayo anakiri hakuwa anaifahamu mwanzo kwenye sentensi zake; – David Kafulila

Nilifikishwa mahakamani kwa kesi mpya ukiachilia kesi ya kwanza ya kupinga matokeo ya uchaguzi 2015 jimbo la Kigoma kusini, awali nilikuwa nikijua ninakesi moja katika mahakama ya hakimu mkazi kigoma kwa madai kwamba nilimdhalilisha aliyekuwa mkuu wa wilaya Khadija Nyembotangu mwaka 2013….nikiwa mahakamani nikapewa tena kesi nyingine ni kesi ya kuhamasisha wananchi wasichangie mchango wa maabara; – David Kafulila

Bado msimamo wagu utabaki palepale kwamba nitaendelea kupigania nchi yangu, kesi hizi zote katika mahakama ya hakimu mkazi Kigoma ukitazama hati za mashitaka yote ya Kafulila hapa Kigoma zimeandaliwa na kusainia na DPP makao makuu Dar es salam inawezekanaje;- Kafulila

Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours