DAVIDO AIKANA ‘MIMBA’ YA MASOGANGE, AELEZA KWA UREFU
Davido amelazimika kuandika maelezo marefu kwenye Twitter kukanusha kuwa ndiye aliyempa ujauzito Agnes Masogange (japo hatujathibitisha iwapo ni kweli mrembo huyo huyo ana mimba). Staa huyo wa Nigeria amedai kuwa boyfriend wa Masogange amekuwa akimpigia simu kwa fujo kulalamika tetesi hizo kuwa huenda akawa analea mimba isiyo yake. “Sijali kuhusu kile blog zinaandika, ukweli au uongo lakini pindi mtu anaponipigia simu kila muda kutoka nchi nyingine akilia kuhusu mchumba wake kuona habari za uongo na anataka kuondoka na kumwacha [Agnes] katika shida,” ameandika. “Haya ni maisha ya watu mnacheza nayo, hadi pale kitu kibaya kitakapotokea kila mmoja ataanza kujisikia kuharibu.  Tafadhali acheni, sio sawa kwa Agnes na mpenzi wake, waacheni waashi na wapate mtoto wao kwa amani,” alisisitiza.
Davido ni mmoja kati ya mastaa wanaodawa kumfaidi mrembo huyo.
Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours