Baadhi ya waathirika wa mafuliko katika kijiji cha mwakata wilaya ya 
kahama mkoani shinyanga wameladhimika kuifunga barabara ya isaka kahama 
na kuathiri kwa muda mawasiliano katika nchi ya rwanda,burundi na uganda
 wakishinikiza serikali kuwagawia chakula,magodoro,branketi.mahema na 
shuka baada ya kunyeshewa na mvua usiku wakati vifaa vya misaada vikiwa 
vimefungiwa kwenye magara hali iliyosababisha jeshi la polisi kuwatawa 
na wananchi kwa mabomu ya machozi na kufungua njia ili gari ziendelee na
 safari.
 
 
 
Naye  mkuu wa mkoa wa shinyanga Bw.Ally Nasoro Rufunga amekabidhi 
misaada hiyo kwa wenyeviti wa serikali za vitongoji na vijiji pamoja na 
kutoa fedha zaidi ya shilingi milioni nne kwa kaya 14 ambapo kila 
familia iliyofiwa imepatiwa kiasi cha shilingi laki tatu kama pole ya 
rambirambi ya serikali ya mkoa wa shinyanga na kuahidi kusaidia zaidi 
kadri misaada inavyopatikana.
Vurugu hizo  zimedumu saa moja ambapo kundi la wananchi wenye 
hasila wakiillamika kamati ya maafa kwa kushindwa kuwahudumia waathirika
 kwa wakati hali iliyosababisha waathirika wanaolala nje kunyeshewa mvua
 huku wakinamama wakila ani nguvu kubwa iliyoumika kutuliza ghasia 
zilizosababisha watoto kupotea kutokana na mabomu ya machozi 
yaliyotumika kutawanya wananchi waliofunga barabara.
Kufuatia vurugu hizo mbunge wa jimbo la msalala Mh.Ezekiel Maige 
ameladhimika kufika kwenye eneo la tukio na kujionea hali halisi ambapo 
amewasihi wananchi kuwa watulivu wakati akifanya mipango ya kuzungumza 
na kamati ya maafa ili iweze kutoa vifaa vinavyolalamikiwa na 
vigawiwekwa walengwa.
Alipotakiwa kujibu malalamiko hayo katibu wa maafa wilaya ya kahama
 ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya ushetu kahama
 Bi.Isabela Chilumba amesema vurugu hizo zinasababishwa na wanasiasa na 
kwamba kamati ya maafa imeba ini kunakundi la vijana kutoka  vijiji 
jirani wakivizia chakula na vifaa vya misaada.


0 comments so far,add yours