
Rais Jakaya Kikwete afanya ziara ya kushtukiza katika eneo la Buguruni Mnyamani ili kujionea madhara makubwa ya mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam na kusababisha zaidi ya watu 1500 kukosa hifadhi baada ya nyumba zao kuingiwa na maji.
Baada ya Rais Kikwete kuwasili  katika eneo hilo la Buguruni 
Mnyamani jijini Dar es salaam huku akizingirwa na umati mkubwa wa 
watu,baadhi ya wakazi hao wamesikika wakipongeza ujio wa rais kufika 
katika eneo hilo ili kujionea walivyokimbia makazi yao baada ya maji 
 kuingia katika nyumba zao na kuwalazimu kulala nje wakilinda mali zao.
Akizungumza na wakazi wa Buguruni Mnyamani,Rais Kikwete amesema 
amelazimika kufika katika eneo hilo ili kuona jitihada zinazofanyika za 
kuondoa maji hayo ili wananchi wawe salama huku akikisisitiza kuwa baada
 ya maji hayo kuondolewa, ujenzi wa bomba mpya ambao ni mkubwa ufanyike 
ili kusaidia kupitisha maji wakati wa mafuriko.
Baadhi ya wakazi wa maeneo hayo akiwemo mzee Saidi Mohamed Bakari 
amesema wanaishi maisha ya tabu na wana siku saba hawajalala kutokana na
 maji hayo kuingia ndani ya nyumba zao.

0 comments so far,add yours