
Muda mfupi baada ya wakuu wa nchi za Tanzania na Kenya kumaliza mgogoro wa kuzuiwa kwa magari ya Tanzania kupeleka wageni katika uwanja wa ndege wa Jomo nchini Kenya magari hayo leo yameanza rasmi safari zao huku wamiliki wasafiri na madereva wakieleza faraja yao baada ya kumalizika kwa mgogoro huo wa kimaslahi.
ITV ilifika katika kituo kikuu cha magari hayo jijini Arusha na 
kushudia magari mengi yakiwa yanaondoka kuelekea Nairobi nchini Kenya 
ambapo wasafiri kutoka nchi zote mbili wamesema maamuzi hayo ni ya 
busara kwani walikuwa wanateseka sana kwa kutumia muda mrefu na wengine 
walilazika kuhairisha safari za kwenda nchi za ulaya na iliwaghalimu.
Kwa upande wao wamiliki wa makapuni yanayotoa huduma hiyo wamesema 
viongozi wa serikali za nchi hizo wametumia busara kubwa kwakuwa tofauti
 hizo zimeathiri uchumi wa watu wengi na madereva nao wakidai walikuwa 
wanapata wakati mgumu katika utendaji wa kazi zao.

0 comments so far,add yours