Wananchi wa kata ya  msanga mkuu wilaya ya mtwara vijijini 
wamelazimika kurudia usafiri wa mitumbwi baada ya kivuko kilicholetwa 
 na serikali miezi miwili iliyopita kusitisha safari zake baada ya 
 kugonga mwamba na kuvunja gia.
Akizungumzia tatizo hilo kaimu meneja wa wakala wa ufundi na umeme 
tamesa mkoa wa mtwara Elitraudi Mmbemba  amesema tatizoli hilo 
limetokana na upepo mkali na hivyo nahodha kukosa mwelekeo na kugonga 
mwamba.
Hata  hivyo amesema hakuna abiria aliyepata tatizo kuhusiana na 
tukio hilo na tayari kifaa hicho kimemepatikana  jijini Dar es salaam na
 wakati wowote kitawasili na kufungwa ili kiendelee na kazi kama 
kawaida.
Wakizungumzia adha  ya kurudia usafiri wa mitumbwi  baadhi ya 
wananchi wa msanga mkuu ambao sehemu kubwa ya maitaji  huyapata mtwara 
mjini wamesema kifaa hicho kiharakishwe mapema kufungwa kusudi waandelee
 na usafiri wao kama kawaida kuliko wanaoutumia wa mtumbwi ambao 
hauaminiki asilimia kubwa. 
kivuko hicho hutumia muda wa dakika 15 kuvusha watu kutoka gati ya mtwara kuelekea ghati ya msanga mkuu.

0 comments so far,add yours