Hatimaye wafuasi 29 kati ya 30 wa chama cha wananchi (CUF) akiwemo naibu mkurugenzi wa oganaizesheni, uchaguzi na bunge Shaweji Mketo na naibu mkurugenzi wa mawasiliano Abdul Kambaya wamepatiwa dhamana huku mmoja ya watuhumiwa hao ambaye ni mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Sandali Bw Abdina Ali Abdina akilazimika kutolewa nje ya chumba cha mahakama baada ya kupata shinikizo la damu kutokana na mdhamini wake kuchelewa kukamilisha taratibu za dhamana.
Shauri hilo lipo mbele ya hakimu Emilius Mchauro wa mahakama ya hakimu mkazi kisutu, jijini Dar es Salaam ambapo wakili wa serikli   Hellen Mushi ambapo kwa upande wa wakili wanaowatetea  washrakiwa hao walinza kuwaongoza washtakiwa hao katika uwasilishwaji wa barua za dhamana na ndipo hakimu alipoanza kuwaoji wadhamini wawatuhumiwa.
 
Zoezi la kuwaoji wadhamini wawatuhumiwa lilipofika kwa mtu wa sita ndipo Bw Abdina Ali Abdina alipo shuhudua mdhamni wake
Akiwa kasimama bila ya barua mkononi ambapo baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo ameelezea hali ilivyokuwa.
 
Baada ya kukamilika kwa taratibu za kidhama wanachama hao walikuwa rumande waliruhusiwa na furaha ilitanda katika viwanja vya mahakama hiyo.
 
Akizungumza katika mahakamani hapo naibu katibu mkuu wa chama hicho Mh Makidalena Sakaya amesema wapo bado wanaendelea
Kuhakisha kuwa wanachama wao wanakuwa huru na jambo kubwa wanaamni ipo siku haki itapatikana.
 
Itakumbukwa kuwa watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani hapo jan 29 mwaka huu wakikabiliwa na mashtaka matatu ikiwemo kufanya mkusanyiko tarehe 27 mwaka huu mkusanyiko wenye nia ya kufanya maandamano kuelekea viwanja vya Zakhiem, Mbagala, Dar es Salaam bila ya kuwa na kibali , shauri hilo litatajwa tena feb 12.
 
Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours