Zaidi ya kaya 1800 katika kata ya Machame Uroki,wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro zimekumbwa na maafa baada ya mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali kuezua mapaa ya nyumba,kungo’a miti mikubwa na migomba iliyokuwa inategemewa kwa chakula.
Wakizungumza kwa masikitiko wananchi wa kijiji cha Uswaa wamesema mvua hiyo iliyonyesha kwa muda wa nusu saa imewaacha katika hali ngumu kimaisha kutokana na mazao ya ndizi yanayotegemewa kwa chakula na biashara kuharibiwa vibaya.
Wananchi hao wamesema kuwa kutokana na hali hiyo iliyotokea katika kata hiyo, wako hatarini kukumbwa na baa la njaa huku wazee wakisema mvua kama hiyo iliyoambatana na upepo mkali iliwahi kunyesha mwaka 1986.
Diwani wa kata ya Machame Uroki Mh.Robson Kimaro amesema hali ya wananchi siyo nzuri kwa kuwa upepo huo pia umeathiri nyumba za ibada na kwamba kata hiyo inahitaji msaada wa chakula .
Kamati ya maafa ya wilaya ya Hai imelazimika kutembelea kata hiyo na kufanya tathmini ya madhara yaliyotokea ambapo mkuu wa idara ya kilimo na maafa amesema kwasasa wanatarajia kuandaa taarifa ya awali na kuiwasilisha ngazi za juu ili kuangalia uwezekano wa kusaidia wananchi hao
Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours