Jana Tanzania iliandika historia katika medali ya soka Afrika na duniani baada ya mshambuliaji Mtanzania anakipiga katika klabu ya TP Mazembe, Mbwana Samatta kushinda tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza Afrika.

Samatta alitangazwa mshindi hukoAbuja, Nigeria katika tuzo zilizowashirikisha mastaa mbalimbali wa soka Afrika.

Furaha ya Watanzania pia imemgusa Rais wa awamu ya tano John Magufuli ambaye ametuma pongezi kwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Nape Nnauye.

Katika taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu Gerson Msigwa, Rais amemtaka Waziri Nape amfikishie salamu za pongezi mchezaji huyo na pia tuzo hiyo imemjengea heshima kubwa na kuleta heshima kwa wachezaji wa Tanzania.

Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours