
Kambi ya upinzani bungeni imeijua juu serikali kwa kitendo chake cha kushinikiza na kutumia ubabe wa kupitisha sheria ambazo ni kandamizi na zenye kubinya na kua uhuru wa vyombo vya habari hatua ambayo imesema inalenga kuliingiza taifa katika giza na kuondoa kabisa dhana ya uwazi ambayo serikali inaihubiri kila mara.
Akisoma hotuba ya kambi ya upinzani bungeni katika wizara ya habari
 utamaduni na michezo Mh Joseph Mbilinyi amesema inashangaza kuona kuwa 
inataka kujiingiza katika mgogoro waandishi wa habari bila ya kuwa na 
sababu yoyote ya msingi.
Aidha kambi ya upinzani imelaani kitendo cha kuwepo kwa vitisho vya
 kutaka kuuwawa kwa mmiliki wa kituo cha ITV Dk Reginalid Mengi kwa 
madai kuwa kituo chake kimekuwa kikitoa habari za uchochezi.
Awali akiwasilisha bajeti ya wizara ya habari utamaduni na michezo 
Mh Dk Fenella Mukangara amesema wizara yake itawasilisha muswada wa 
sheria ya huduma za habari ambapo ukipita utasaidia kuweka misingi imara
 katika sekta ya habari.
Lazaro Nyalandu ni waziri wa maliasili na utalii ambaye naye 
amewasilisha bajeti yake nakubainisha mipango mbalimbali yakiwemo   
namna ya kupambana na ujangili.
Kwa upande waziri kivuli wa wizara hiyo mchungaji Peter Msigwa 
ameitaka serikali kuteketeza shehena ya pembe za ndovu ambazo 
imezikamata ili kuipunguzia serikali mzigo wa gharama wa kutunza pembe 
hizo.

0 comments so far,add yours