
Kiongozi wa kanisa katoliki nchini 
Mwadhama Polycarp  Kadinali  Pengo  amewataka wakristo kote nchni 
kumuomba mungu aliepushe taifa na  matukio ya ubaguzi, vita, ugaidi  na 
mauaji yanayotokea Duniani ikiwemo mauaji ya kikatili ya wanafunzi 
waumini wa kikristo yaliyotokea katika  chuo kikuu cha Garisa nchini 
Kenya.
 
 
Akizungumza katika ibada ya Jumatatu ya Pasaka iliyohudhuriwa na 
mamia ya wanachama wa shirikisho la kwaya katoliki nchni, Kadinali Pengo
 pia amewataka wakristo nchini kumuomba mungu asafishe hali 
iliyojitokeza nchini Kenya na kuwataka kuwawajasiri na kubaki katika 
misimamo ya imaniya  kikristo kwa kutamka ukweli  iwapo hali hiyo 
italazika kujitokeza.
Aidha kuhusu katiba inayopendekezwa,Padinali Pengo  amesema kama 
kiongozi wa  Dini hawezi kurudia au kubadilisha kauli aliyokwisha itoa 
kwa wananchi,kwani kufanya hivyo kutaweza kusababisha ugomvi ambapo 
amewataka waumini wa kanisa katoliki kusambaza kauli hiyo kote nchni.
 Awali kiongozi wa kanisa katoliki nchini Mwadhama Polycarp 
 Kadinali  Pengo ametaka wananchi waachiwe wasome katiba inayopendekezwa
 na kufanya maamuzi wenyewe.

0 comments so far,add yours