Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dr Reginald Mengi amesema kujiajiri ni 
miongoni mwa dawa za kumaliza tatizo la ajira kwa vijana kwa vile 
Serikali na sekta binafsi haina uwezo wa kuajiri vijana wote wanaohitimu
 vyuoni kila mwaka nchini.
Mwenyekiti Mtendaji wa  IPP, Dk Reginald Mengi ameyasema hayo 
jijini Dar es salaam wakati akikabidhi  ruzuku ya shilingi milioni 10 
 kwa mshindi wa kwanza kwa Mwezi Januari , Bw. Frederick Shayo, wa 
shindano la wazo la biashara analoliendesha kupitia twita yake kwa mwezi
 Januari.
Akikabidhi zawadi hiyo Dr Mengi amewataka vijana na wananchi 
kubadili fikra na kuamini kuwa kwa kutumia fursa  na raslimali za taifa 
wanaweza kubuni mawazo bora ya kufanya ujasiriamali utakaowawezesha 
kujikwamua kiuchumi na kusisitiza kuwapuuza watu  wanaodai kuwa Tanzania
 haihitaji mamilionea.
Dr Mengi pia amewazawadia  shilingi milioni moja kila mmoja 
washiriki tisa   waliofanikiwa kuingia kumi bora. Washindi hao ni  Jesse
 Temba, Charles Kapondo, Gerald Nyaisssa, George Rashid, na Otaigo 
Elisha. Wengine ni  Alphonce Mallya, Japhet Bachu, Kibanga Omari, na 
Emmanuel Buberwa.
Wazo la mshindi wa kwanza lilikuwa kukarabati majokofu mabovu 
kuyageuza kuwa viatamishi rahisi vinavyotumia umeme mdogo kwa ajili ya 
wafugaji wa kuku.

0 comments so far,add yours