Serikali mkoani Singida imewaagiza wakurugenzi watendaji wa 
halmashauri za wilaya pamoja na wakuu wa wilaya wote mkoani Singida, 
kuhakikisha wanafuatilia miradi inayo anzishwa na iliyo kwisha anza 
kufanya kazi, ili miradi hiyo iwe endelevu na kuwa saidia wananchi, 
tofauti na sasa miradi mingi imekuwa haiendelei.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dk .Parseko Kone ametoa agizo hilo wakati 
alipokuwa akiwakabidhi wakuu wa wilaya mashine ishirini nanne  za 
kufyatulia matofali ( intetlocking blocks ) zilizo tolewa na shirika la 
nyumba la taifa kwa ajilia ya kusaidia makundi ya vijana kujiajiri.
Awali akiongea kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa shirika la nyumba la
 taifa, meneja wa NHC mkoani Singida Bwana Ladislaus Bamanyisa  amesema 
shirika la NHC limelenga kupunguza tatizo la makazi hapa nchini ifikapo 
mwaka elfumbili na kumina tano kwa kujenga nyumba za beinafuu nchi 
nzima, pia mashine hizo zina lenga kupunguza tatizo la ajira kwa vijana 
hapa nchini.

0 comments so far,add yours