IMG-20131119-00045Anaitwa Gabriel Munissi mkazi wa Mwanza ambae Polisi Ilala Dar es salaam ilithibitisha kwamba ndio amehusika kufanya mauaji ya watu wengine wawili kabla ya yeye kujiua huku ikiaminika ni kutokana na wivu wa kimapenzi.
Kama hukuipata hii taarifa ni kwamba Gabriel alikwenda Ilala na kusimama nje ya nyumba moja iliyokua na fensi na geiti jeusi kusubiria atoke Mwanamke anaetajwa kuwahi kuwa mpenzi wake na kisha baada ya Mwanamke huyo kutoka huku akiendeshwa na mwanaume mmoja kwenye Toyota Surf na kukiwa na abiria wengine wawili kwenye gari, Gabriel ndio alianza kufyetua risasi ovyo.
Shahidi alieshuhudia hili tukio mwanzo mwisho anasema waliamini kabisa kwamba Gabriel hakuwa jambazi kwa jinsi alivyoshambulia na kuendelea kubaki eneo la tukio bila kuwadhuru watu wengine waliokuwemo karibu, vilevile kama angekua jambazi isingekua rahisi kwa yeye kujiua.
Shuhuda anasema Gabriel alipiga risasi mpaka zilizokuwa ndani zikaisha ikabidi aongeze nyingine na kuendelea kushambulia huku akiwa hana nia ya kuwaua wale abiria wengine kwenye gari baada ya kuwajeruhi isipokua Mwanaume aliekua anaendesha pamoja na Mwanamke anaetajwa kuwa mpenzi wake ambae alikua amekaa pembeni ya dereva.
 Gabriel Munissi
Waliouwawa kwenye tukio hilo wanatajwa na polisi kuwa ni mwanaume aliekua anaendesha gari pamoja na mdogo wa Mwanamke anaetajwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Gabriel.
Baadhi ya marafiki wa Gabriel Mwanza wanasema Gabriel ni miongoni mwa vijana wa mjini waliokua wanaishi vizuri kwa kuendesha magari ya kifahari na kuwa na pesa za kutosha hivyo pesa haikua tatizo kwake.
millardayo.com kila siku inakuhudumia kwa kukupa habari za matukio mbalimbali ya kisiasa, muziki, michezo, movies, maisha na kila kitu muhimu inachoona unapaswa kukipata zikiwemo pichaz za matukio mbalimbali hivyo ili kuwa Mwanafamilia unaweza kujiweka karibu zaidi ya facebook.com/millardayo twitter.com/millardayo na instagram.com/millardayo ili kupata kila tukio kiganjani mwako.
Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours