RAIS wa Marekani, Donald Trump ameilaani Korea Kaskazini kwa kitendo cha ukatili kutokana na kifo cha mwanafunzi mmoja wa Marekani, Otto Warmbier.
Trump alisema   kifo cha Warmbier kimeimarisha mipango ya utawala wake ya kutaka kuwatetea wengine dhidi ya  majanga kama hayo katika mikono ya mataifa yasiyoheshimu sheria.

”Marekani kwa mara nyingine inashutumu ukatili wa utawala wa Korea Kaskazini huku tukimkumbuka mwathiriwa wa hivi karibuni,” alisema Trump.
Mwanafunzi huyo aliachiwa huru baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 15 na alikuwa ameshikiliwa   Korea Kaskazini kwa miezi 15.  Alifariki dunia siku sita tu baada ya kuachiliwa
Korea Kaskazini ilimrudisha Marekani Warmbier wiki iliopita ikidai kuwa alikuwa hana fahamu kwa  mwaka mmoja na kwamba ilikuwa ikimsaidia kibinadamu.
Warmbier ambaye alihukumiwa kwa kujaribu kuiba bango la propaganda kwenye hoteli moja nchini humo, hakuweza kupata fahamu tena.
Familia yake imelaumu  kifo hicho katika kile ilichokiita unyanyasaji mkali dhidi ya mtoto wao alipokuwa akishikiliwa na maofisa wa usalama wa Korea Kaskazini.
Akielezea hali ya kijana huyo, alisema alikuwa katika hali ya kutojitambua   alipoachiliwa kutoka jela na kuanzia hapo alilazwa hospitalini kwa matibabu.
Madaktari waliokuwa wakimtibu kijana huyo walisema  alikuwa na majeraha makubwa ya kuumia mishipa ya fahamu.

Share To:
Magpress

MagPress

Vestibulum bibendum felis sit amet dolor auctor molestie. In dignissim eget nibh id dapibus. Fusce et suscipit orci. Aliquam sit amet urna lorem. Duis eu imperdiet nunc, non imperdiet libero.

0 comments so far,add yours