Jeshi la polisi mkoani Mara limezima  
maandamano ambayo  yameitishwa na Chama cha demokrasia na  maendeleo 
Chadema  wilayani Bunda  mkoani Mara,huku viongozi  kadhaa  wa  chama  
hicho   wakikamatwa na jeshi  la  polisi  kwa  madai  ya  kukaidi  amri 
halali ya jeshi hilo.
Askari wa jeshi la polisi wakiwemo wa kikosi cha 
kutuliza ghasia wa FFU wakiwa  katika  magari manne  tofauti walianza  
kufika katika mji wa Nyasura wilayani Bunda eneo ambalo lilipangwa na 
Chadema  kunzia maandamano hayo, kisha  kutolewa  kwa  amri   ambayo  
iliwataka  wafuasi hao wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali 
kutawanyika mara moja katika eneo hilo.
Hata  hivyo  baada  ya  baadhi  ya  wafuasi  na    
viongozi  hao   wa  Chadema  kukaidi   amri  hiyo, polisi  walianza  
kurusha  mabomu  ya  machozi  kisha kuwakamata watu  kadhaa  wakiwemo 
viongozi  chama  hicho   wilaya  ya Bunda.
 wakizungumzia hali hiyo  baadhi  ya viongozi  wa 
chadema  wilaya ya bunda,wamelalamikiwa  hatua ya  jeshi la polisi  
kutumia  nguvu  kubwa kuzima maandamano hayo  ambayo  wameyaita  kuwa 
ya  amani.
Naye  kamanda wa polisi mkoani Mara ACP Philip Alex
 Kalangi,akizungumza kwa njia ya simu amesema jeshi la polisi 
limewakamata watu kumi  wakiwemo viongozi  wa chama hicho  wilayani 
Bunda  kwa kushindwa  kutekeleza agizo  la jeshi  hilo  lilowata 
kusitisha  maandamano hayo  ya  kupinga  kuendelea  kwa bunge  la  
katiba  ambalo amesema  linaendeshwa kwa  mujibu  wa  sheria.


0 comments so far,add yours