Jeshi la polisi mkoa wa Morogoro limewashushia kipigo baadhi ya wafuasi wa Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema na kutumia mabomu kuwatawanya wanachama waliokuwa wakijiandaa kufanya maandamano katika ofisi ya Chadema mtaa wa Ngoto mjini Morogoro.
Askari wajeshi la polisi walionekana kwa wingi 
kuzunguka ofisi za Chadema za mjini Morogoro ambapo wafuasi wa Chadema 
walikua katika maandalizi ya kufanya maandamano huku wakionekana na 
mabango ya kupinga kuendelea kwa vikao vya bunge la katiba ambapo kabla 
ya mandamano hayo  baadhi ya vijana walipigwa na kisha kupakizwa katika 
gari la jeshi la polsi ambapo baadhi ya viongzi wa Chadema wamelalamikia
 jeshi la polisi kutumia nguvu huku wengine wakilalamikia baadhi vifaa 
vya ofisi kupote wakati wa vurugu hizo.
Katika hatua nyingine baadhi ya askari wa jeshi la 
polisi walitaka kuingia kwa nguvu katika ofisi za Chadema kuwachukua 
baadhi ya watuhumiwa walio kuwa wakifanya vurugu ambapo walizuiwa na 
viongozi wa Chadema na mambo yalikua hivi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Lenard Paul 
akizungumzia tukio hilo amekiri jeshi la polisi limetumia mabomu 
kuwatawanya wafuasi wa Chadema na wamelazimika kufanya hivyo kwa kua 
walikua wakiandamana bila kufuata utaratibu kwa kukika maagizo 
yaliotolewa na jeshi  la polIsi nchini na katika tukio hilo watu watano 
wanashikiliwa na wamefikishwa mahakamani.HAPO JUU PICHANI NI
Ndugu wa marehemu Ally Nzona akiwa amesimama kando ya mwili wa ndugu yake katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro, ambaye alifariki kwa kupigwa risasi na polisi wakati wa maandamano ya amani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mjini Morogoro

0 comments so far,add yours